
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
February 5, 2025 at 05:47 PM
Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh,
Tunapenda kuwaletea mrejesho wa maendeleo ya programu yetu ya Ramadhani. Tunawashukuru wote waliojisajili na wanaoendelea kushiriki katika mpango huu wa kheri.
Tafadhali hakikisha unakagua malipo yako ili kuhakikisha yamefika kama ulivyotuma. Ikiwa kuna tatizo lolote, usisite kuwasiliana na viongozi wetu kwa msaada.
Kwa wale ambao bado hawajajiandikisha, tunawahimiza kufanya hivyo mapema ili kufanikisha mpango huu kwa ufanisi. Pia tunawakumbusha wale waliokwisha jisajili kuanza kulipia pack zao kulingana na ahadi walizotoa.
Tunaomba ushirikiano wenu ili kufanikisha jambo hili kwa baraka za Allah.
Jazakumullah khayran.