
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
February 20, 2025 at 06:37 PM
NURU YA RAMADHANI
Ramadhani ni mwezi mtukufu uliojaa baraka, rehema, na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni wakati wa kujitakasa, kujikurubisha kwa Allah, na kuimarisha imani kwa njia ya swaum, dua, sadaka, na ibada nyengine nyingi.
Katika mwezi huu, Waumini hufunga kuanzia alfajiri hadi machweo, wakijizuia na chakula, kinywaji, na matendo yasiyompendeza Allah. Funga si tu kujizuia na njaa na kiu, bali pia ni mafunzo ya subira, taqwa, na ukaribu na Mola wetu
👍
1