IMANI MAWAIDHA CHANNEL
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
February 23, 2025 at 06:42 PM
Tusihukumu watu tunapowaona wakirejea msikitini kipindi cha Ramadhani kwa ajili ya ibada. Badala ya kuwasema vibaya au kufichua mapungufu yao ya zamani, tuwapokee kwa moyo wa upendo na tuwaunge mkono katika jitihada zao za kumrudia Mola. Kila mmoja ana safari yake ya imani, na Ramadhani ni wakati wa rehema na msamaha. Tuwe daraja la kuwaongoza kwa wema badala ya kuwavunja moyo.

Comments