IMANI MAWAIDHA CHANNEL
IMANI MAWAIDHA CHANNEL
February 25, 2025 at 03:40 AM
Asalam alaykum warahmatuAllah wabarakat. _Nasaha za ramadhani-05_ Makosa Tunayofanya Ndani ya Ramadhani: Kusahau Swalah ya Alfajiri Miongoni mwa makosa ambayo wengi wetu tunajikuta tukifanya ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kushindwa kuswali Swalah ya Alfajiri kwa wakati wake. Hili hutokea hasa pale tunapojitahidi kuswali Taraweh kwa uangalifu mkubwa, kisha baadaye tunaamka kwa ajili ya Tahajud na kula daku, lakini baada ya hapo tunarudi kulala na hatimaye kusahau au kushindwa kuamka kwa ajili ya Alfajiri. Ni muhimu kuelewa kwamba ingawa ibada ya Taraweh na Tahajud zina fadhila kubwa, Swalah ya Alfajiri ni faradhi isiyo na mbadala. Mtume ﷺ amesema: "Swalah nzito zaidi kwa wanafiki ni Swalah ya Isha na Alfajiri. Na lau wangelijua fadhila zake, basi wangelizihudhuria hata kwa kutambaa." (Bukhari na Muslim) Hivyo basi, tujitahidi kupanga muda wetu vyema, ili tuhakikishe kuwa Swalah ya Alfajiri haitupiti. Tukumbuke kwamba faradhi ina uzito mkubwa zaidi kuliko sunnah, na mafanikio ya Ramadhani ni katika kuzitimiza ibada zote kwa usahihi na kwa wakati wake. Khayrat Imani groups +254758794104 +255696925298
🙏 1

Comments