
Yuvinus Live
February 23, 2025 at 01:35 PM
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene ameipongeza timu inayosimamia mchakato wa ajira za Ualimu kwa namna wanavyoendesha zoezi hilo kwa uadilifu na ufanisi.
Mhe. Simbachawene amesema hayo tarehe 22 Februari, 2025 wakati alipotembelea na kukagua timu inayosimamia mchakato wa ajira za Ualimu Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) Mkoani Morogoro.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaita ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo Viongozi wa vijana waliojitambulisha kwenye andiko lao kuwa ni “Non Employed Teachers Organisation (NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya Kijamii.
“Nimesoma Makala yao yenye kichwa cha habari Ombi la Wahitimu wa Ualimu Vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo” alisisitiza Mhe. Simbachawene.
Aliongeza kuwa amewasiliana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adol