
TBS - Viwango
February 26, 2025 at 07:45 PM
_Energy Drink_ inaweza kuongeza nishati na nguvu mwilini kutokana na kuwa na kafeini na sukari kwa kiwango cha juu, hata hivyo ikitumiwa bila kufuata maelekezo inaweza kusababisha athari kama vile kuongezeka kwa mapigo ya moyo, shinikizo la juu la damu, na upungufu wa maji mwilini, utegemezi wa kafeini na kukosa usingizi. Pia mchanganyiko wa vichocheo katika __Energy Drinks_ _unaweza kuwa na madhara kwa watu walio na matatizo ya kiafya hivyo ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi.