THE  JKUAT LENS:::Quad Chronicles...juja Vibes💯🔥
THE JKUAT LENS:::Quad Chronicles...juja Vibes💯🔥
March 1, 2025 at 07:23 AM
♥️ SECRETS ♥️ SN02 Chapter 09🦋 So nikapata Stesh amepuke bedroom mzima💔. Nilishtuka nikashindwa what's going on na nikitoka alikua tu fiti Me : Beb what's going on🤔 Stesh : Sijui beb..i just feel unwell Me : Tuishie hosy? Stesh : Maybe 🥹 Tukajipiga kwa dinga hadi hosy. Nikachill hapo nje nitegee atibiwe. Nurse akatokea huko Nurse : Hello are you Mr Carl? Me : Yeah Nurse : Ooh wewe ni nani wake Kisubmarine ukiskia swali kama hio ujue you are ready to donate a kidney😂💔 Me : I'm her bo... Nurse : Ooh boyfriend.. okay.. Stesh has malaria and some stomach ulcers..atalazwa leo then probably by Tuesday usiku shell be okay Me : it's okay 😟 Wueh i thought hadi angenishow ako na ball😂. Sikukua ready kukua baba😂. So nikaishia ward alipelekwa tukakaa na yeye hapo. Akanijenga key nifike kwake nimletee towel na jacket. Kufika sikupata mtu. Hata dinga ya Blake haikukua. Nikajipiga kwa hao nikachomoa hizo stuff. Kuingia keja ya Blake haina hadi viatu zake nikajua mzee maybe alibanja majuu. Nikarudi hosy. Giza ilikua imeshika Stesh : Beb but we utareport kwa job kesho usirisk kufutwa kazi Me : Don't worry beb i gatch you Nilidoz hapo kwa bed yake hadi morning. Nikaishia kwa hao. Kufika tu hivi Ras akanicall 📱 Ras : Carl Me : Yooh Ras : Change of roles.. unajua we unakaa mjanja kiasi kushinda hizi kondoo mbili..niko sure hata hio form ungepiga solo haingeharibika..ilimess ju haukukua..hakuna form tumepiga na wewe ikasink Me : 😂😂😂 Ras : kuanzia leo wewe ndo supervision wa hawa majamaa wawili kwa hio job yetu.. calls zote za form zitakua zinapitia kwako sasa ni wewe uwapange Me : Eii man but hapo Cliff ataanza kunichukia bro Ras : Hawezi jua😂..this is our secret hawezi shikanisha.. Me : Okay 😂 Ras : Nataka tugawane hizi doo leo afternoon Me : wazi Ras : Yeah nimebonga na Denno..then ulipata zile doo nilikurefund? Me : Yeah bro shukran So mzee nimepandishwa cheo😂. Nikapiga shower nikakimbia tao nikabuy fruits supa na mastuff kathaa nikapelekea Stesh hosy. Hio day niliingia job kaa nimechelewa. The first person kupatana na yeye alikua Celine Celine : Mmh yani message yangu hadi sahi bado haijakua replied Me : I'm sorry nilisahau Celine : Carl sio ati nakutaka but I'm just jealous.. unajua you gave me a certain vibe kama mse ako ready to settle with me..like you were pretending as if you are into me.. actually i was not happy about that Me : Ooh huyo dem?.. she's a friend alikua anadai nimpeleke mahali so vile nilikata akajam..huyo anakuaga hivo ako na attitudes zingine sijui za wapi..na by the way you look se°xy today kwani rada😂 Celine : 😂😂😂sikuamini Me : Trust me. Celine : Anyway thanks for the complement. What are you doing today after job? Me : Niko tu Celine : Maybe this se°xy dress might end up in your house🤣🤣 Me : We'll see Dem akanijenga hug akarudi huko juu. Kuangalia huko ju nacheki curtain ya dirisha ya Damian iko open kiasi like kuna mse anachungulia nikajua ni yeye 😂💔. Nikaanza job. 11am hapo Damian akaniita Damian : Bro dinga zimekam..nataka tuishie wewe na Denno ziletwe Me : Wazi Jamaa alikua anakaa kubonda mbaya sana😂💔. Kulikua na chupa glani hapo akagongesha hadi ikapasuka😂. Tukaishia tukaleta madinga mbili. Dinga zilikua brandy mbaya sana. Ile yenye hata nzi ikiland juu inaslide hadi chini😂💔. Damian akapewa yake then ya Cliff ikamtegea pale kwa slot. Damian : Alafu Carl unajua Mike alikuleta hapa na ni morio wangu sana..usifanye nikosane na yeye Me : Bro kwani noma ni gani..hadi nimekaa for long bila kupatana na mike Damian : Unacheki sasa..mkisaidiwa mnasahau wasee waliwasaidia..nakumbuka ukikam hapa Carl hadi haukua na anything sahi uko na madoo unakohoa kama Mike sonko unabeba kichwa kama ya mudavadi Me : Buda sasa umeanza matusu Damian : Saka mike hadi umshukuru bana💔 Me : Sikatai but mbona unasema nitakukosanisha we na Mike Damian : Carl unajua we ukiona tu manzi yeyote hapa hata haujui nimemtoa wapi unamdai tu..sijui ni nini hua inakusumbua..ama unacompete na mimi?🤔.. ulikua kwa Jessy sahi ni Celine Me : Wueh..buda mi hizi story za kupigania madem sidai..hapa tuko job bro..yani hadi siwezi bonga na manzi kwa kazi unaona tu namdai Damian : I saw the way she was laughing at you bro hio sio kicheko ya kanisa..lazma kuna mambo hapo.. I'm putting an eye on you.. Me : Na wewe vile ulikua unadai Tresh nilibonga?..ni mara ngapi umeniona na Tresh?..what if sahi niambie hawa madem unaringia ati ulikua unasimp kwa Tresh hadi unambuyia flowers? Damian : Mind your tongue bro hio information umetoa wapi Jamaa akaanza kushout. Nikajua hapa ni suspension ingine ya kimataifa. Akakunja shirt akanisongea. Kisubmarine pia mimi nikaivisha mkono ikae ready Damian : Bonga tena niskie bonga mse Denno : Yooh bro rada nini inahappen hapa manze unapiga kelele hadi the other side Celine : Gai Carl what's going on😟 Damian : Toka nionyeshe huyu mse vumbi Me : Bro unajiweka joto sijui ni ya wapi maze tulia Damian : Denno niwache uone mse akinuka kichinjio sahi kwani huyu mse anathani ye ni nani Denno : Carl kwani nini imehappen jooh Me : Damian ametokea tu huko na vishasha mi hadi sielewi Denno kuzubaa Damian akanirukia kaa amenishika kwa shingo. Sikutaka kufight na yeye ju najua anasaka kitu ya kunifutia job. Jamaa akaanza kuninyonga. Nikamtoa mkono. Akanifeed ngumi flani imekula ugali ya wimbi💔. Nikahepa ngumi kaa tano but moja ikaland kwa forehead karibu avunjike vidole. Soldier akakuja kumtoa hapo Soldier : Hapana manze lakini wewe Damian ni mchokozi nimekua nimekaa pale tu nacheki kila kitu haufanyi fiti bana hii ni job Denno : Damian hapo umechoma maze Celine : Like mbona ufanye ivo Damian and you are like our boss Damian : Nitokee kwa njia msee ama nikutoke magoti Jamaa akamatch akarudi kwa ofisi yake. Celine akaboil maji kwa electric kettle akanimassage kwa uso. Me : Si ungenishow tu mapema huyu mse hukudai Celine : Whaat🙁..kwani ni mimi anapigania? Me : We uliza..kuanzia leo there's nothing between me and you.. sidai kupoteza job Celine : Carl surely just like that?.. there's nothing between me na Damian maybe he has been admiring me lakini mimi siwezi sema we have a connection niskize Carl sasa hata Damian naenda naye wapi Nikarudi kwa dinga nikachill. Kiasi hivi kwa navigation nikacheki kuna mse anadai kubebwa. TO BE CONTINUED 🔥 *@veetheteller*
😂 1

Comments