GLOBIFY
GLOBIFY
February 17, 2025 at 06:30 AM
*GLOBIFY CHARITY* Globify Charity Ni Kundi La WhatsApp Linalojitolea Kusaidia Jamii, Hususani Watoto Yatima Na Watu Wenye Mahitaji Maalum Kupitia Michango Ya Hali Na Mali Ya Wajumbe. Kundi Hili Ni Sehemu Ya Mtandao Mpana Na Mzuri Wa Magroup Ya WhatsApp Yanayojulikana Kama *Globify*, Ambayo Yalianzishwa Na *Ndugu Issa Halili Issa* Kwa Lengo La Kuunganisha Watu Kwa Ajili Ya Shughuli Mbalimbali Za Kijamii, Kiuchumi, Kisiasa Na Kitamaduni. Globify Charity Imefanikiwa Kusaidia Vituo Mbalimbali Nchini Tanzania Na Zanzibar, Vikiwemo: 1. *Kituo Cha Bibi Na Babu (BABIWA)* - Madale, Dar Es Salaam (Jan 31, 2024) 2. *Kindness Orphanage Centre* - Kijenge, Arusha (Apr 7, 2024) 3. *Irente Orphanage Home* - Lushoto, Tanga (28 Jul 2024) 4. *Islamic Yatima Foundation* - Ilemela, Mwanza (Oct 13, 2024) 5. *Salim Turky Foundation* - Kiwengwa, Kaskazini Unguja, Zanzibar (Dec 8, 2024) Mwaka 2025 Globify Charity Imejipanga Kutembelea Vituo Vingine Ili Kuendelea Kutoa Misaada Mbalimbali Kwa Kuanza Na Kituo: 6. *Tumaini Foundation* - Chang'ombe - Ihumwa, Dodoma (2025) Globify Charity Imejikita Katika Kusaidia: ➖Kutoa Vifaa Vya Malazi, Chakula, Mavazi Na Vifaa Vya Kielimu. ➖Kutoa Ushauri, Nasaha Na Kuimarisha Huduma Za Michezo Kwa Watoto Ili Kuchangia Maendeleo Yao Ya Kimwili Na Kiakili. Globify Charity Inaamini Katika Kujenga Maisha Bora Kwa Watoto Na Jamii Kupitia Hisani, Umoja, Mshikamano Na Upendo. https://chat.whatsapp.com/BiYVpSHVGt34tTA2eMQA3z *GLOBIFY CHARITY, LET LOVE CONNECT US*

Comments