
Tanzania National Parks
May 29, 2025 at 12:37 PM
๐๐
๐๐๐๐๐ ๐๐๐
๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐
๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐๐๐
๐๐. ๐๐ฌ๐๐ฃ๐๐๐จ๐๐ ๐ฌ๐๐ฉ๐ช - ๐๐๐๐ค๐ง๐.
Hifadhi ya Taifa Mto Ugalla ni miongoni mwa hifadhi tano mpya iliyoanzishwa mwaka 2019 baada ya sehemu ya Pori la Akiba la Mto Ugalla na Hifadhi ya Misitu Ugalla Kaskazini kutengwa rasmi kuwa Hifadhi ya Taifa. Hifadhi hiyo iko katika Mkoa wa Tabora, Magharibi mwa Tanzania na ina eneo la takribani kilomita za mraba 3,865.
๐๐๐ฃ๐๐๐๐ง๐ ๐ฃ๐ ๐๐๐ฏ๐๐ฃ๐๐๐ง๐.
Hifadhi hii ina mandhari ya kipekee yenye mchanganyiko wa misitu ya miombo, Savana zenye nyasi fupi (Zambezian flooded Grassland), misitu ya vichaka iliyosheheni miti aina ya Mihama, mabonde na milima. Mto Ugalla ambao unapita katikati ya hifadhi hii, ni chanzo muhimu cha maji kwa wanyamapori hasa wakati wa kiangazi na maji yake huelekea Magharibi hadi eneo la ardhi oevu ya Moyowosi ambayo hutiririsha maji yake kupitia mto Malagarasi kuelekea Ziwa Tanganyika.
๐๐๐ฃ๐ฎ๐๐ข๐๐ฅ๐ค๐ง๐.
Hifadhi ya Taifa Mto Ugalla ni makazi ya aina mbalimbali za wanyama wakiwemo Tembo, Simba, Chui, Twiga, Tandala wakubwa, Pofu, Nyamera, Pundamilia na Nyati. Pia, hifadhi hiyo ina idadi kubwa ya makundi ya swala aina ya palahala (Sable) na Korongo (Roan Antelope) ambao ni nadra kupatikana kwa pamoja sehemu nyingine nchini isipokuwa Hifadhi ya Taifa Ruaha ambayo ina sifa zenye uoto wa asili unaofanana.
Vilevile, hifadhi hii ina wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka kama vile Mbwa Mwitu. Katika maeneo ya mabwawa na mito unaweza kuona viboko, Mamba na aina mbalimbali za ndege adimu wa majini kama vile Korongo domo kiatu (Shoebill stork) na ndege wakazi na wahamao.
๐๐๐ช๐๐๐ช๐ก๐ ๐ฏ๐ ๐๐ฉ๐๐ก๐๐.
Watalii wanaotembelea hifadhi hii wanaweza kufurahia shughuli mbalimbali za utalii kama vile utalii wa magari, matembezi ya miguu, utalii wa kutazama ndege (birds watching), pia hifadhi inatarajia kuongeza mazao mengine ya utalii kama kuvua samaki na kuachia (sport fishing, canoeing na hiking) kwenye maeneo ya milima.
๐๐ช๐๐๐ ๐๐ ๐ ๐ ๐ฌ๐๐ ๐.
Hifadhi hiyo hufikika kwa njia ya barabara kutoka Tabora kupitia Urambo, Kaliua umbali wa takribani kilomita 180 kufika hifadhini, kwa njia ya Anga kwa kushukia katika Kiwanja cha Ndege Tabora sanjari na viwanja vitatu vidogo (airstrip) vilivyopo ndani ya Hifadhi hiyo. Pia kwa watalii wanaopenda kusafiri kwa njia ya treni hifadhi hii ni mahali pake.
Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hiyo ni msimu wa kiangazi kuanzia Julai hadi Novemba ambapo wanyama wengi hukusanyika kando kando ya Mto Ugalla na mito mingine ya msimu kujipatia maji na malisho. Kwa wakati huo nyasi za maeneo hayo huwa ni za kijani tofauti na maeneo ya mbali na mto ambapo nyasi zake huwa ni kavu na rangi ya kahawia.
๐๐๐ก๐๐ฏ๐ ๐ฃ๐๐๐ฃ๐ ๐ฎ๐ ๐๐๐๐๐๐๐.
Watalii wanaotembelea hifadhi hiyo watapata huduma za malazi kwenye (Special campsite) ziliyotengwa na hifadhi kwa ajili ya kupiga mahema pamoja na maeneo mengine manne kwa ajili ya โFly Campsiteโ. Aidha, TANAPA inawaalika wadau na wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza katika malazi na mazao mengine ya utalii kama vile utalii wa Puto (Baloon).
๐
๐
๐
4