Rhapsody Global Club ( Mandate 1B ROR Influences )
Rhapsody Global Club ( Mandate 1B ROR Influences )
June 8, 2025 at 08:15 PM
Rhapsody Swahili Mon Jun 09 2025 NGUVU YA UHUSIKA MKUU Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu… (Yohana 1:41-42). Katika kazi ya kuendeleza Ufalme wa Mungu, wahusika wakuu wanahitajika, na tunaona kwamba kulikuwa na watu kama hao katika Biblia, hasa katika Injili ya Yohana. Hawa hawakuwa wafuasi wa Yesu Kristo tu bali ni wahamasishaji hai (vinara) wa huduma Yake. Matendo yao yanadhihirisha namna fulani ya kazi maalum—uhusika mkuu katika ubora wake. Kwa mfano, katika Yohana 1:40-42, tunaona Andrea, mmoja wa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji ambaye aliacha kila kitu ili kumfuata Yesu. Andrea hakubaki nao mwenyewe ufunuo huu mpya alioupata. Alimtafuta mara moja kaka yake, Simoni (Petro), akamwambia, “Tumemwona Masihi!” Kisha akamleta Petro kwa Yesu. Matendo ya Andrea yanaonyesha moyo wa kiongozi wa kweli—mtu ambaye anaendeleza na kutangaza huduma ya Yesu kwa kuwaleta wengine kujiunga na kusudi Lake na kutekeleza kazi Yake. Siku iliyofuata, Yesu alimwita Filipo ili amfuate. Filipo naye, kama Andrea, hakubaki na Habari Njema mwenyewe. Akampata Nathanaeli, akasema, “Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari Zake katika torati na manabii, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yusufu.”(Yohana 1:45) Nathanaeli, akiwa na mashaka mwanzoni, aliuliza, “Je, kitu chochote kizuri kinaweza kutoka Nazareti?” Jibu la Filipo lilikuwa rahisi, lakini lenye nguvu; alimwambia Nathanaeli, “Njoo uone” (Yohana 1:45-46). Hii ni nguvu ya kuongoza. Andrea na Filipo hawakumfuata Yesu tu, bali walileta wengine Kwake. Waliunganisha Wayahudi wenzao na walio wacha Mungu, ambao tayari walimwamini Mungu, kuja kwenye kusudi la Masihi. Vile vile, katika kueneza Ufalme wa Mungu leo, tunahitaji jeshi kubwa la watu wa Mungu waliojitolea, wenye shauku na wasiolegea katika utume wa Injili. Tunatimiliza kikamilifu kuhubiri Injili mwaka huu wa 2025. Kuwa mhusika mkuu wa agizo hili! Walete na uwahimize wengine kujiunga na kazi hii tunapotimiza Agizo Kuu. Ni jambo la lazima kwetu kutambua kwamba ili kuleta mabadiliko katika ulimwengu, tunahitaji jeshi lenye umoja la Wakristo, kila mmoja atekeleze sehemu yake katika kuendeleza Ufalme wa Mungu, hasa kwa kuwa kurudi kwa Bwana kunakaribia. Prayer / Confession Baba Mpendwa, ahsante kwa kunifanya kuwa mhusika mkuu katika kuendeleza Ufalme Wako. Kupitia mimi, wengi wanaletwa katika Ufalme na kujumuishwa katika jeshi Lako kuu, wakitimiza kusudi Lako la kiungu na kubadilisha maisha ya watu kila mahali. Ninatembea katika hekima na nguvu za Roho, daima nikisambaza ushawishi wa Ufalme, katika Jina la Yesu. Amina. Further study Yohana 1:40-42; Yohana 4:28-30; 2 Timotheo 2:2 1-year bible reading plan Matendo ya Mitume 1:1-26 & 2 Mambo ya Nyakati 1-4 2-year bible reading plan Marko 16:1-11 & Kumbukumbu la Torati 7 WhatsApp Chanel for rhapsody Translation : https://whatsapp.com/channel/0029Va9SJ9OHFxP0Xh4KCN3F

Comments