
UFUNDI KITANDANI❤️👙😍
May 27, 2025 at 07:43 AM
NINI UNATAKIWA KUFANYA BAADA YA KUPEWA NAMBA NA BINTI.
Moja kati ya purukushani za kiume ni kuomba namba kwa binti ambaye umevutiwa naye. Hili ni swala gumu kiasi hasa unapokutana na binti mtata .
Sasa baada ya kupambana na binti huyo kukupa namba kinachofuata ni kumueleza swala lako na akuelewe, hii ni changamoto nyingine ambayo ni kubwa zaidi.
Kwanza unatakiwa kuelewa, binti akikupa namba maana yake ameona kwa namna fulani unamfaa na unaweza kuwa naye katika mahusiano, kwahiyo kizingiti cha kwanza umekivuka na sasa unatakiwa usiharibu ili kuvuka kizingiti cha pili ili umpate kama kusudio lako.
Ukiona binti kakupa namba halafu badae akaacha kukuonyesha ushirikiano na akakupotezea kwa asilimia kubwa umeshindwa katika hatua ya pili ya kumuingia sasa, yani baada ya kupewa namba ulifanya nini? Hapa ndipo penye jambo.
Sasa hebu tuone baada ya kupewa namba ni nini unatakiwa kufanya.
1. MUUNGE NA BANDO LA SMS, DAKIKA AU DATA.
Baada ya kupewa namba muulize angependa umuunge na bando lipi kati ya sms, dakika na data, lakini kubwa wewe angalia kama utakuwa unamtafuta kwa sms za kawaida muunge sms, na kama utakuwa unamtafuta WhatsApp muunge data.
Usiwe mshamba bro, hivyo vimeseji vyako vya mambo! Umeamkaje! Anakujibu kwa salio alionunuliwa na nani?.
Humuungi kifurushi kwakuwa hana ila kwa kuwa unatengeneza mazingira ya kujibiwa. Unatafuta mamlaka kwake.
2. MUULIZE ANAPENDELEA AINA IPI YA MAWASILIANO.
Hapa namaanisha kama anapenda kupigiwa au kuchati, kuna mtu hapendi kupigiwa ila sms tu, na kuna mwingine ni mvivu wa kuchati anataka kupigiwa.
Yajue haya yote ili usimkere mtu.
3. MUULIZE MUDA GANI ANAKUWA HURU KUWASILIANA NA WEWE.
Sio tu kwakuwa kakupa namba basi unapiga kila muda, sms kila dakika. Kuwa mstaarabu, kuwa na mipaka kwakuwa bado huna mamlaka naye.
4. USIMTONGOZE PUNDE TU BAADA YA KUPEWA NAMBA.
Bro huyo binti anatongozwa kila siku, ashasikia kila neno la mwanaume, kwahiyo wewe kumtongoza sio kitu kipya, lakini pia wewe kumuomba tu namba tayari anajua kinachofuata, kwahiyo kuwa tofauti.
Jenga mazoea ya kumjulia hali na kuwasiliana naye angalau mara tatu kwa siku, mzoeshe hivyo kwamba unamcheki kila siku. Muulize vitu anavyopenda na asivyopenda, kwa kifupi mfahamianae kwa undani.
Acha kumuuliza kama ana mtu au hana, hayo anajua yeye na atakwambia mwenyewe kama atataka, kikubwa fanya majukumu yako, siku zote mwanamke anahitaji mwanaume wa tofauti, ukiwa na vigezo kuliko mtu wake hiyo nafasi utapata.
5. MPE ZAWADI.
Muulize size ya mguu wake, size ya kiuno chake halafu mnunulie zawadi katika hayo mawili. Hii michakato yote inaonyesha unamtongoza ila wewe umekuwa tofauti tu na watongozaji wengine ambao wanaweka maneno meengi mbele.
6. TAFITI NA UJUE SIFA ZAKE.
Kama utashindwa kujua sifa zake za ndani basi hata sifa za nje tu. Katika mazungumzo yenu uwe unamwambia unapenda mwanamke wa aina hii na ile, ila katika hiyo aina ya mwanamke huyo weka sifa zake yeye.
Mfano yeye ni mweupe, basi mwambie unapenda mwanamke mweupe, au mwembamba basi mwambie unapenda mwanamke mwembamba, hapo yeye anakuwa najua tu unachomaanisha na anakuwa anakuchora tu.
7. MTOE OUT.
Muombe muende kwa chakula cha usiku, kama atakubali nendeni mkale, mnywe na mfurahi, pigeni story zingine tu wala usimtongoze, ila usisahau kumwambia amependeza sana, unajua kwanini? Mwanamke akiwa anatoka out huwa anavaa vizuri hivyo kutomwambia amependeza utakuwa umeiharibu siku yake vibaya mno.
Siku hiyo msalimie kwa kumkumbatia, halafu baada ya kumaliza kumbatio hilo hapo hapo mwambia umependeza sana, halafu muangalie usoni uone tabasamu lake.
Kama nilivyokwambia siku hii wala usimtongoze, ongeeni mambo mengine tu.
Baada ya hizo hatua zote na kuzoeana vizuri, sasa mwambie unavutiwa naye na ungependa kuwa naye. Msisitize pia kuwa unaamini hutapata jibu tofauti na matarajio yako.
❤️
😂
🙏
3