RadioTehranSW
June 9, 2025 at 04:23 AM
*MATANGAZO YA JUMATATU ASUBUHI RADIO TEHRAN:*
Iran: Tuko tayari kuimarisha uhusiano na Ulaya lakini kwa kuheshimiana
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi anasema kuwa, Tehran iko tayari kupanua uhusiano na nchi za Ulaya hususan Italia lakini kwa sharti la kuheshimiana na kulindwa maslahi ya pamoja.
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127352-iran_tuko_tayari_kuimarisha_uhusiano_na_ulaya_lakini_kwa_kuheshimiana
Jeshi la Somalia laangamiza makamanda kadhaa wa al-Shabaab
Makamanda watatu waandamizi wa kundi la kigaidi la al-Shabab walioendesha wimbi la mashambulizi mabaya nchini Somalia katika miezi ya karibuni wameuawa katika operesheni ya pamoja ya usalama.
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i127350-jeshi_la_somalia_laangamiza_makamanda_kadhaa_wa_al_shabaab
Iran: Vikwazo vya US dhidi ya majaji wa ICC vinakirihisha
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei amekosoa vikali hatua ya Marekani ya kuwawekea vikwazo majaji wanne wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutokana na uchunguzi wao juu ya uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127348-iran_vikwazo_vya_us_dhidi_ya_majaji_wa_icc_vinakirihisha
"Kuuawa viongozi wa Muqawama kunaimarisha irada ya Wapalestina"
Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imelaani vikali mauaji ya Israel dhidi ya afisa mashuhuri wa Muqawama na watu wengine 30 katika mji wa Gaza na kusisitiza kuwa, mauaji hayo yanayolenga viongozi wa mrengo wa mapambano kamwe hayatadhoofisha uthabiti na azma ya wananchi wa Palestina.
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127346-kuuawa_viongozi_wa_muqawama_kunaimarisha_irada_ya_wapalestina
Umoja wa Mataifa: Gaza imegeuka na kuwa Jahannamu; njaa inaondoka na roho za watoto
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, yakiashiria kwamba mpango wa Marekani na Israel wa kusambaza misaada huko Gaza una hatari kubwa, yamesisitiza: Gaza imekuwa jehanamu ya kweli na sasa njaa inatishia maisha ya watoto wasiopungua 71,000.
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i127344-umoja_wa_mataifa_gaza_imegeuka_na_kuwa_jahannamu_njaa_inaondoka_na_roho_za_watoto
*UCHAMBUZI WA KISIASA:*
Namna kujiunga Iran na Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS kunaweza kubadilisha maingiliano ya kifedha na kibenki
Mohammad Reza Farzin, Gavana wa Benki Kuu ya Iran, amekutana na Dilma Rousseff, Rais wa Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS katika kikao cha magavana wa benki kuu na mawaziri wa uchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Beijing na kujadiliana naye kuhusu kuimarishwa maingiliano ya kifedha na kibenki na nchi wanachama wa kundi hilo.
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127342-namna_kujiunga_iran_na_benki_mpya_ya_maendeleo_ya_brics_kunaweza_kubadilisha_maingiliano_ya_kifedha_na_kibenki
*Leo ni Jumatatu tarehe 13 Mfunguo Tatu Dhulhija 1446 Hijria sawa na Juni 9 mwaka 2025 Milaadia.*
Siku kama ya leo miaka 1957 iliyopita inayosadifiana na tarehe 9 Juni mwaka wa 68 Miladia, Mfalme Nero Claudius Caesar mtawala katili na aliyemwaga damu nyingi wa Rome alijiua, baada ya kuishi kwa miaka 31 na kutawala kwa...
https://parstoday.ir/sw/radio/programs-i127340-jumatatu_juni_9_2025