TUCASA STU
TUCASA STU
May 16, 2025 at 09:56 PM
*DAR NET EVENT 2025-NURU YA MATUMAINI.* *SIKU YA 07/21.* *WINFRIDA MITEKARO.* *KAYA NA FAMILIA.* *SOMO: MSAMAHA.* Jana tuliona somo la suala la migogoro. Wakati mwingine migogoro huwepo kati ya watu inaweza kutokana katika mtazamo wa kimaisha. Leo tunazungumzi Msamaha. *Kanuni kubwa ya kutatua migogoro katika familia ni MSAMAHA.* *Msamaha ni nini? Ni Uamuzi wa kuacha chuki na mawazo ya kulipiza kisasi.* *"Iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma mkisameheana kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi." Waefeso 4:32.* *1. WAZO LA KUSAMEHE LINATOKAΝΑ ΝΑ MUNGU* Mungu katika bustani ya Edeni. Mwanzo 3:15. Mungu alichukia dhambi lakini upendo wake ulikuwa palepale hata Adamu na Hawa kuanguka. *2. KUSAMEHE SI JAMBO RAHISI.* *Hasa ikiwa mtu aliyekuumiza hakubali makosa.* *Maisha yanaweza kuumiza! Na kufanya iwe vigumu kusamehe nakuendelea kushikilia msamaha kwa muda mrefu.* 3. MUNGU ANATAMANI WATOTO WAKE WAISHI KWA KUSAMEHEWA NA KUENEZA MSAMAHA KWA WENGINE Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. Mathayo 6:14-15. 4. MSAMAHA HUDHIHIRISHA KUWA UMEBADILISHWA NA MUNGU. Msamaha huja kama matokeo ya unyenyekevu na kuponywa kwa nafsi. 5. MSAMAHA NI MCHAKATO. #. Hisia za msamaha zinaweza zisije hapo hapo, kulingana na kina cha maumivu. Lakini wakati ni mganga mkubwa #. Tunapoendelea kumwendea Mungu, Yeye hutupatia uponyaji na roho ya msamaha. #. Hatupaswi kuhisi hatia kwa sababu maumivu hayaondoki mara moja. Hata hivyo, tunapokuwa na uzoefu wa kuumizwa lazima tupambanie kuwa huru kama Yusufu, na kuwasamehe kwa dhati wale waliotuumiza. #. Tunapojikabidhi kwa Roho Mtakafu tunawekwa huru. Usiposamehe unaendekeza chuki. Usiwe katika utumwa kwa sababu ya kutosamehe, SAMEHE. 06. MSAMAHA SIYO KAMA BIASHARA. Hatupaswi kumngojea aliyetukosea atuombee msamaha ili tumsamehe. Stefano alipokuwa anapigwa mawe, bado aliwaombea msamaha wa watesi wake (Matendo 7:54-59). *7. MSAMAHA SIYO KUFUMBIA MACHO MAKOSA.* Anayesamehe, hutambua kuwa kosa limefanyika. Msamaha unahusisha kumsamehe mkosaji bila ya kukubaliana na kosa. "Wala mimi sikuhukumu; nenda wala usitendedhambi tena." (Yohana 8:11) 08. KATIKA KUSAMEHE LAZIMA USHUGHULIKE. Usiruhusu maumivu yakufanye uwe na uchungu na kupoteza imani kwa Mungu pamoja na wanadamu wote. *Paulo anashauri: "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na viondolewe kwenu," (Waefeso. 4:31-32.* Mfanye mtesi wako awe mradi wako wa maombi. Yesu anasema: "Wabarikini wanaowalaani waombeeni wanaowaudhi" Luka 6:28. *KATIKA KUSAMEHE LAZIMA USHUGHULIKE.* Kumwombea adui hakuleti tu mabadiliko kwa adui, bali hufanya maajabu pia kwa yule anayeomba. Mwombe Mungu mahususi kwa ajili ya neema yake ya kudumu ya kukuona kwenye maumivu. Usikalie sana maumivu bali ruhusu Mungu afanye kazi ndani zaidi yako kupitia hayo maumivu. Tukiangalia kwa makini tutaona kile ambacho Mungu anajaribu kufanya kwa ajili yetu na ndani yetu. 09. KUNA FAIDA KATIKA KUSAMEHE. Kesho tutaendelea kujifunza juu ya faida za kusamehe. Usikose kesho na Mungu akubariki. Andika majina ya watu uliowakosea kisha Omba Mungu akusamehe na Mungu awasamehe pia ili uwe huru na wao wawe huru. *MUNGU ATUBARIKI SOTE.* 🙏🙏🙏🙏
🙏 ❤️ 3

Comments