TUCASA STU
TUCASA STU
June 6, 2025 at 03:04 AM
*KESHA LA ASUBUHI 2025.* *IJUMAA, JUNI 6, 2025.* *KILA SIKU ONGEA MANENO YA KRISTO.* *Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli.-Yohana 8:31.* ▶️ Ni mapenzi ya Mungu kwamba kila akiriye kuwa Mkristo akamilishe tabia inayoshabihiana na ile ya Mungu. Kwa kujifunza tabia ya Yesu iliyofunuliwa ndani ya Biblia, kwa kuweka katika vitendo wema Wake, aaminiye atabadilishwa katika mfanano huo huo wa fadhili na rehema. Kazi ya Kristo ya kujikana nafsi na ya dhabihu vikiletwa katika maisha ya kila siku vitakuza imani itendayo kazi kwa upendo na kutakasa nafsi. Kuna wengi ambao wanatamani kukwepa sehemu ya kuubeba msalaba, lakini Bwana anawaambia wote Anaposema, "Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate" (Mathayo 16:24). ▶️ Kazi kubwa inapaswa kukamilishwa kwa kuzitangaza kweli za Biblia zinazookoa. Hii ndiyo njia iliyoamriwa na Mungu ili kukomesha wimbi la upotovu wa maadili duniani. Kristo alitoa maisha Yake ili kufanya iwezekane kwa mwanadamu kurejeshwa kwa sura ya Mungu. Ni nguvu ya neema Yake inayowaleta watu pamoja katika kuutii ukweli. Wale ambao wanataka kupata uzoefu wa utakaso wa ukweli katika nafsi zao wenyewe imewapasa kuwasilisha ukweli huu kwa wale wasioujua. Kamwe hawatapata kazi ya kuinua na kuadilisha zaidi kama hii.... ▶️ Hakuna mtu anayefanywa kufaa kwa kazi hii isipokuwa anajifunza kila siku kuongea maneno ya Mwalimu aliyetumwa toka kwa Mungu. Sasa ndio wakati wa kuotesha mbegu ya injili. Mbegu tunayoipanda lazima iwe ile ambayo itazalisha matunda bora zaidi. Hatuna muda wa kupoteza. Kazi ya shule zetu inapaswa kufanana zaidi katika tabia kama kazi ya Kristo. Ni nguvu tu ya neema ya Mungu inayofanya kazi katika mioyo na akili za wanadamu ambayo itafanya na kuweka mazingira ya shule na makanisa yetu kuwa safi.... ▶️ Katika ujumbe ambao umetumwa kwetu mara kwa mara, tuna ukweli ambao utatimiza kazi ya ajabu ya matengenezo katika tabia zetu ikiwa tutaupatia nafasi. Utatuandaa kwa ajili ya kuingia katika mji wa Mungu. Ni fursa yetu kuendelea daima hata kufikia daraja la juu la maisha ya Kikristo.... 🔘 *Tunahitaji kubadilishwa kutoka kwenye maisha yetu maovu hata kuiamini injili. Wafuasi wa Yesu hawahitaji kujaribu kung'aa. Ikiwa watadumu kuyatazama maisha ya Yesu watabadilishwa katika akili na moyo hata kufikia mfanano Wake. Kisha watang'aa pasipo kujaribu kung'aa. Bwana hataki tuwe na maonesho ya wema. Katika karama ya Mwanawe amefanya uwezekano kwamba maisha yetu ya ndani yajawe na kanuni kutoka mbinguni. Ni upokeaji wa utoaji huu ambao utaongoza katika ufunuaji wa Kristo kwa ulimwengu. Watu wa Mungu wanapopata uzoefu wa kuzaliwa upya, ukweli wao, unyofu wao, uaminifu wao, kanuni zao thabiti, zitayadhihirisha hayo bila kushindwa (Counsels to Parents, Teachers, and Students, 249-251).* *MUNGU AKUBARIKI SANA.* 🙏🙏🙏🙏
🙏 1

Comments