
Exim Bank Tanzania
June 11, 2025 at 06:27 AM
Asante sana kwa wafanyakazi wa Benki yetu, wateja pamoja na wanajamii wote walioungana nasi kwenye zoezi la uchangiaji damu! ❤️🩸
Zoezi hili limefanywa na Benki yetu kwa Kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) katika mikoa mwishoni mwa wiki hii katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Shinyanga-Kahama, na wiki hii Zoezi la kuchangia Damu litaendelea katika mikoa ya Mbeya na Mtwara. Sambamba na kuchangia Damu tumekabidhi jumla ya vifaa 110 muhimu vya kimatibabu kwa NBTS. Dhamira yetu ikiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa damu salama na kuweza kuokoa maisha ya Watanzania.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Bi. Kauthar D’souza, Meneja Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki yetu, alisisitiza, “Huu ni mpango wa kitaifa wa uchangiaji damu, sio tu Dar es Salaam, bali unafanyika pia Dodoma, Mtwara, Kahama na Mbeya, kwa lengo la kuongeza kiasi cha damu itakayokusanywa ikilinganishwa na mwaka jana."
Kwa upande mwingine, Bi. Judith Charle, Msimamizi wa Huduma za Wachangia Damu kutoka NBTS, alielezea shukrani zake za dhati kwa ushirikiano huu unaoendelea. “Tunashukuru sana kwa msaada na ushirikiano na Benki ya Exim kwa miaka mingi sasa. Ushirikiano wao ni muhimu katika kutusaidia kuziba pengo la upatikanaji wa damu kwani tunaamini kila damu inayokusanywa, na kila kifaa kinachotolewa, kinamaanisha moja kwa moja maisha ya Mtanzania yanaokolewa mahali fulani.”
Benki yetu inaendelea kuwa mshirika thabiti katika maendeleo ya kitaifa, ikiwekeza daima si tu katika ujumuishaji wa kifedha na uvumbuzi, bali pia katika sekta muhimu kama afya, elimu, na ustawi mpana wa jamii.
