
Hussein Ali Mwinyi
June 7, 2025 at 02:25 PM
Nimeshiriki katika Baraza la Eid Al Adha lililofanyika leo, tarehe 7 Juni 2025, katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein – SUZA, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika Baraza hilo nimewahimiza Waislamu kuzingatia mafunzo yanayotokana na ibada ya Hijja, hususan utii kwa Mwenyezi Mungu, mshikamano, na maadili bora ya kijamii katika kuilinda amani ya dini ya Kiislamu.
Aidha , nimesema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwawezesha wananchi wengi zaidi kutekeleza ibada hiyo muhimu, ikiwemo kuharakisha uanzishwaji wa Mfuko wa Hijja, pamoja na kuwezesha safari za moja kwa moja za ndege kutoka Zanzibar hadi Saudi Arabia.
Vile vile, nimewahimiza viongozi wa dini na wananchi wote kuiombea Zanzibar iendelee kuwa na amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu kwa kueleza kuwa mazingira ya utulivu ni nguzo muhimu ya kuimarisha maendeleo ya jamii.
🙏
❤️
👍
👏
😂
8