Samawati Safari
Samawati Safari
June 9, 2025 at 06:49 AM
[03] Kigali, Rwanda – Mauaji ya Kimbari ya Watutsi (1994) Katika kipindi cha siku 100 pekee mwaka 1994, takribani watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda. Mauaji haya ya kinyama yalihusisha majirani kuwaua majirani, wake kuuawa mbele ya waume zao, na watoto kuuliwa mbele ya wazazi wao. Hutu waliyochochewa na chuki ya muda mrefu dhidi ya Watutsi walitumia mapanga, marungu na silaha za kienyeji kusambaza mauti. Dunia iliangalia kimya kimya, ikishindwa kuzuia janga hili la aibu. [04] Nanking, China – Mauaji ya Nanking (1937) Baada ya jeshi la Japan kuvamia mji wa Nanking mwaka 1937, wakazi wa mji huo walikumbwa na mateso ya kikatili. Kwa muda wa wiki sita, askari wa Kijapani waliua takribani watu 300,000 kwa njia za kinyama – wakibaka wanawake, kuua watoto, na kuchinja raia kama wanyama. Historia ya Nanking ni somo la jinsi vita vinavyoweza kuharibu utu wa mwanadamu.
Image from Samawati Safari: [03] Kigali, Rwanda – Mauaji ya Kimbari ya Watutsi (1994)  Katika kipi...

Comments