
Samawati Safari
June 9, 2025 at 06:51 AM
[07] Darfur, Sudan – Mauaji ya Kimbari (2003–leo)
Darfur ni eneo lililogeuka kuwa jangwa la mauti tangu mwaka 2003.
Vikosi vya serikali ya Sudan vikishirikiana na wapiganaji wa Janjaweed walishambulia jamii za kabila la Fur, Masalit na Zaghawa.
Zaidi ya watu 300,000 walifariki, na mamilioni kupoteza makazi yao. Mauaji haya yamekuwa ya muda mrefu, yakisindikizwa na ubakaji wa wanawake na uharibifu wa makusudi wa maisha ya kijamii.
![Image from Samawati Safari: [07] Darfur, Sudan – Mauaji ya Kimbari (2003–leo) Darfur ni eneo lili...](https://cdn2.wapeek.io/2025/06/12/08/07-darfur-sudan-mauaji-ya-kimbari-2003-leo-darfur-ni-eneo-lililogeuka-kuwa-jangwa-la-mauti-tangu-mwaka-2003-vikosi-vya-serikali-ya-sudan-vikishirikiana-na-wapiganaji-wa-janjaweed-walishambulia-jamii-z_66e6ed100b9a1721761f41c67010f2f8.webp)
😮
1