Samawati Safari
Samawati Safari
June 11, 2025 at 06:35 AM
Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION). Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa. Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.
Image from Samawati Safari: Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bun...

Comments