Samawati Safari
Samawati Safari
June 11, 2025 at 06:37 AM
Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo. Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja. katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Comments