
Samawati Safari
June 11, 2025 at 08:07 PM
Walimuita Anna, lakini mitaani walimzoea kwa jina la "Dada Poa wa Buguruni." Alikuwa maarufu – si kwa uzuri wake tu, bali kwa namna alivyokuwa mcheshi, mkarimu, na mwenye roho ya kusaidia.
Alikuwa dada ambaye, licha ya maisha aliyoyachagua, aliishi kwa misingi ya utu na heshima. Alikuwa ni sura ya ukimya wa mateso ambayo jamii haikuweza – au haikutaka – kuyaona.
Anna alizaliwa mwaka 1996 huko Mtwara, mtoto wa pili katika familia ya watoto watano
Baba yake alifariki akiwa mdogo, na mama yake alihangaika kuwasomesha. Alifika kidato cha tatu, lakini maisha yalikuwa magumu.
Baada ya mama yake kuugua ugonjwa wa muda mrefu, Anna aliacha shule na kwenda Dar es Salaam "kutafuta maisha".
Ndipo alipofika Buguruni, mtaa uliojaa kelele, ndoto zilizovunjika, na mianga ya usiku ambayo haijui mchana.
Anna aliingia katika maisha ya kuuza mwili akiwa na miaka 19.
Alijipatia wateja kupitia baa za Buguruni, hasa maeneo ya rozana . Alijua namna ya kuvuta macho ya wanaume – si kwa mavazi tu, bali kwa tabasamu la uongo lililoficha huzuni ya maisha.
Lakini tofauti na dada poa wengine, Anna alikuwa na ndoto. Alihifadhi sehemu ya hela zake, akisaidia ndugu zake kijijini.
Aliota kufungua saluni. Kila alipokuwa amelewa, aliwaambia rafiki zake:
"Mimi siishi hivi milele. Siku moja nitaondoka hapa."
Siri Aliyoibeba