Samawati Safari
Samawati Safari
June 11, 2025 at 08:08 PM
Juni 2021, Anna alifariki dunia akiwa kwenye chumba kidogo alichopanga Buguruni . Hakukuwa na mtu wa familia karibu, zaidi ya Zena na dada mmoja wa jirani aliyekuwa akimuosha. Alizikwa kwa msaada wa watu wachache waliompenda kwa dhati – wauza chips, mama wa baa, na madereva bajaji waliokuwa wanamjua kama "yule dada poa mcheshi." Hakuna aliyepiga picha. Hakuna gazeti lililotangaza kifo chake. Hakuna mchungaji wala shehe aliyemfahamu. Lakini wale waliomjua walimwomboleza kwa kimya – kimya kikali kama kifo chake.
Image from Samawati Safari: Juni 2021, Anna alifariki dunia akiwa kwenye chumba kidogo alichopanga...

Comments