
Samawati Safari
June 12, 2025 at 06:28 AM
Mwaka 2010, Tundu Lissu aliingia rasmi katika siasa alipogombea na kushinda Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia chama cha CHADEMA.
Akiwa bungeni, alijitokeza kama mmoja wa wabunge wachache waliokuwa jasiri, wanaosema ukweli hata mbele ya mamlaka kuu.
Aliibua hoja nzito kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma, mikataba ya madini isiyo na manufaa kwa taifa, na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Msimamo wake wa wazi ulivuta macho ya umma na kumfanya kuwa kiongozi mashuhuri wa upinzani.
Mambo hayakuwa mepesi.
Alikamatwa mara kadhaa, alishambuliwa kwa maneno makali kutoka kwa viongozi wa serikali, lakini hakuyumba.
