Abdulsamad Channel
May 30, 2025 at 05:57 PM
Leo nlifika nyumbani kwa familia ya marehemu Sheikh Jabir Haidar Kikwajuni nikiambatana na Maafisa wa Ubalozi wa Brazil na Balozi mdogo mwenzangu wa Msumbuji mwenye makaazi yake Zanzibar Mhe.Agostino Abacar Trinta kutoa mkono wa pole na kuwafariji watoto wa marehemu na wafiwa.
Aidha, niliwataka wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na subira katika kipindi hichi kigumu cha msiba mzito pamoja na kuwasihi kuendeleza yale yote mazuri ya marehemu Jabir, ikiwemo sadaka zake pamoja na kuendelea kumuenzi marehemu kwa Dua, sadaka na visomo mbali mbali.
Innalillah Wainailaihi Rajiun. Tunamuomba Allah amsamehe, ampe kauli thabit, nasi atupe khatma na mwisho mwema. Amen