
Abdulsamad Channel
June 1, 2025 at 11:32 AM
Jana Jumamosi ya Mei 31, 2025 baada ya Salat Ishaa nilijumuika na waumini wenzangu wa Kiislamu tukiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, katika Dua na kisomo cha khitma kwa ajili ya kumuombea marehemu Sheikh Jabir Haidar Jabir Al-Farsy. Dua hii ilifanyika katika Msikiti wa Weles uliopo Kikwajuni na kusomwa na Ustadh Abdulrahman Mwinyi Dedes.
Marehemu Sheikh Jabir wakati wa uhai wake alikuwa muumini mkubwa wa dini, mwalimu na mwanaharakati wa masuala mbali mbali ya Dini ya kiislamu.
Tulipata fursa ya kusomewa Wasifu mzuri wa marehemu uliosomwa mbele wa viongozi, waumini na wanafamilia yake, vijana wa Tarika kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo masheikh mbali mbali walihudhuria kisomo hicho.
Tunamuombea Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema Peponi, amsamehe madhabi yake na alitie Noor kaburi lake. Amin!
Inna Lillaahi wa Inna Ilayhi Rajiu'n.

🙏
1