Samia Suluhu Hassan

Samia Suluhu Hassan

737.8K subscribers

Verified Channel
Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan
May 14, 2025 at 04:50 PM
Katika kazi hii leo, nilipomkaribisha nchini Rais wa Finland, Mheshimiwa Alexander Stubb. Tanzania na Finland zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano uliojengwa katika misingi ya urafiki, maelewano na kuheshimiana. Ziara hii ni hatua ya nchi zetu kuendelea kuimarisha ushirikiano huo ambao matunda yake tumeendelea kuyaona katika sekta za utawala bora, elimu na utunzaji mazingira. Tumejadili na kukubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta zinazogusa maisha ya watu wetu kama vile uchumi wa buluu, nishati, elimu na teknolojia. Aidha, nimetumia nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara alioambatana nao kuangalia fursa za biashara na uwekezaji nchini.
🙏 👍 ❤️ 😢 😮 😂 591

Comments