Samia Suluhu Hassan

Samia Suluhu Hassan

737.8K subscribers

Verified Channel
Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan
May 31, 2025 at 02:11 PM
Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana. Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali. Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano.
Image from Samia Suluhu Hassan: Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bun...
❤️ 🙏 👍 😂 😢 😮 1.5K

Comments