
Samia Suluhu Hassan
June 8, 2025 at 02:15 PM
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya ndugu zetu 28 na majeruhi 8, vilivyotokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku katika Mlima Iwambi, kwenye Barabara Kuu ya Tanzania - Zambia, Mkoa wa Mbeya.
Ninawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone haraka. Aidha, ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Homera, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyenzi Mungu awajalie subra na uvumilivu.
Ninawasisitiza madereva kuendelea kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani. Nimeliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria za usalama barabarani, na pia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuendelea kuboresha hali ya barabara zetu, hasa maeneo yenye changamoto kubwa zaidi, kwa usalama wa watumiaji wote wa barabara.
😢
🙏
❤️
👍
😂
😮
1.1K