
Samia Suluhu Hassan
June 9, 2025 at 03:23 PM
Katika jukumu muhimu la kuhakikisha ulinzi na usalama ndani ya nchi yetu, leo nimeshiriki sherehe ya kufunga mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi 954 wa Jeshi la Polisi. Idadi hii ni kubwa zaidi ya wahitimu kwa mara moja, tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) mwaka 1961. Nimempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Camilius Wambura kwa mafanikio haya ya kujivunia yanayolenga kuimarisha jeshi letu katika majukumu yake.
Nimewapongeza na kuwaasa wahitimu kutumia ujuzi na uelewa walioupata kujibu changamoto za kiutendaji pamoja na kuchochea maboresho na mabadiliko ndani ya jeshi hilo katika utoaji huduma kwa wananchi. Kazi yao hii muhimu pia izingatie haki, maadili na ushirikiano na jamii, pamoja vyombo vingine vya ndani na vya nchi nje ya nchi katika kudhibiti uhalifu na wahalifu.
🙏
❤️
👍
😂
😮
😢
426