MKINGU NATURE RESERVE (Eco Tourism Area )
MKINGU NATURE RESERVE (Eco Tourism Area )
June 3, 2025 at 06:01 PM
_Pango la Mzee Malolo_ Pango hili linapatikana ndani ya hifadhi ya mazingira asilia mkingu, Pango hili linasifika sana kwa kuwa na historia ya kuvutia inayomuhusisha mzee malolo Ambae ni mzee maarufu aliyewahi kuishi katika kijiji cha _mafuta_ kabla ya kuondoka na kuingia msituni na kuanza maisha yake mapya ndani ya pango hilo. Pango hili linasifika kuwa na vyumba vikubwa vya kumuwezesha mtu kuishi humo akiwa na familia bila wasiwasi. _Je wajua ni sababu ipi iliomfanya mzee huyu wa ajabu kukimbia na kuishi katikati ya msitu ?_🤔 _Je unafahamu maajabu ya shamba la mzee malolo ?_🤔 _Je unafahamu maisha ya mzee huyu akiwa katikati ya msitu mnene wa kutisha.?_🤔 😳 _Je aliwezaje kuishi humo pangoni na vipi kuhusu mahitaji? alifanikiwa vipi kupambana na changamoto za msitu unaotisha na viumbe wa ajabu?_ 🤔 Majibu yote ya historia ya pango la mzee malolo utayapata ufikapo hifadhi ya mazingira Asilia Mkingu. *Karibu Ufahamu historia karibu utalii mkingu.*
Image from MKINGU NATURE RESERVE (Eco Tourism Area ): _Pango la  Mzee Malolo_  Pango hili linapatikana ndani ya hifadhi ya m...

Comments