TBS -  Viwango
TBS - Viwango
June 2, 2025 at 06:28 PM
Afisa Udhibiti Ubora (TBS),Bi. Sarah Maro akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali waliohudhuria maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa yaliyofanyika katika viwanja vya zimamoto Manispaa ya Morogoro. Bi. Maro aliwasisitiza wananchi kuhusu umuhimu wa kusoma taarifa zinazopatikana katika vifungashio vya bidhaa kabla ya kununua bidhaa husika hususani muda wa mwisho wa matumizi.
👍 1

Comments