Rhapsody Global Club ( Mandate 1B ROR Influences )
Rhapsody Global Club ( Mandate 1B ROR Influences )
June 13, 2025 at 06:56 PM
Rhapsody Swahili Sat Jun 14 2025 NGUVU YA MAONO NA KUFIKIRI KWA PICHA Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo fito… (Mwanzo 30:37). Hadithi ya Yakobo katika Mwanzo 30 na 31 ni dhihirisho la kuvutia la uwezo wa maono na kufikiri kwa kuona picha. Wakati Yakobo alikubali kufanya kazi kwa Labani, aliahidiwa ng'ombe kama mshahara. Hata hivyo, Labani alibadili masharti na kumdanganya Yakobo mara kwa mara. Lakini Yakobo, kupitia hekima ya Mungu na mkakati wa kuumba, aligeuza hali hiyo. Yakobo akatwaa vijiti vya miti mibichi ya mlubna, na mlozi, na mwaramoni, akamenya mistari myeupe juu yake, ili kuifanya ile nyeupe ionekane. Akaziweka fimbo hizo kwenye vyombo vya kunyweshea maji ambako mifugo walikuja kunywa maji. Wanyama hao walipopandana mbele ya fimbo hizo, walizaa watoto ambao ilikuwa vile vile kama Yakobo alivyotaka. Baadaye, Yakobo hakuhitaji tena fimbo hizo. Akawatenga wanyama, wenye marakaraka na mabakamabaka na kuwaweka mbele ya wanyama wenye nguvu. Kwa kufanya hivyo, alitengeneza maono kwa ajili ya mifugo, na wakazaa kulingana na kile walichoona. Mbinu ya Yakobo ilikuwa dhihirisho la uwezo wa maono katika uumbaji. Alitumia uwezo wake wa kufikiri kwa picha ili kulazimisha matokeo. Ng’ombe wenye nguvu walipochukua mimba, Yakobo aliweka zile fimbo mbele ya macho yao, akihakikisha kwamba watazaa watoto wenye nguvu na wa kuvutia. Ng’ombe walipokuwa dhaifu, hakutumia fimbo hizo, kwa hiyo wale waliokuwa dhaifu zaidi walikuwa ni wa Labani. Baada ya kitambo, mifugo ya Yakobo ilizidi kuwa na nguvu na mingi zaidi, ilihali mifugo ya Labani ilibaki dhaifu. Mafanikio ya Yakobo yalikuwa kwa ufunuo wa kiungu. Katika ndoto, aliwaona mabeberu wote wanaowapanda wanyama wenye milia, na madoadoa, na marakaraka. Malaika alithibitisha maono haya, akisema, “...Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka…” (Mwanzo 31:12c NKJV). Jinsi hili lilivyo la muhimu! Una uwezo wa kuunda siku zijazo kuwa unavyotamani kwa kuzingatia kile unachotaka kuona. Tengeneza maono unayotaka kwa ufahamu wako. Kupitia Neno na nguvu za Roho Mtakatifu zinazofanya kazi ndani yako, unaweza kuunda au kutengeneza uhalisi wa maisha yako. Haleluya! Prayer / Confession Baba Mpendwa, ahsante kwa kunipa uwezo wa kuona na kuunda maisha yangu yajayo ninayotamani kupitia nguvu ya maono na Neno Lako. Ninapotumia uwezo wangu wa kufikiria, nikiongozwa na Roho Wako, ninajenga maisha yangu kulingana na kusudi Lako la kimungu, kwa ushindi na upanuzi katika kila nyanja. Nimewezeshwa kuathiri ulimwengu wangu na kutimiza hatima yangu, katika Jina la Yesu. Amina. Further study Mwanzo 13:14-17; Habakuki 2:2; Waefeso 3:20 1-year bible reading plan Matendo ya Mitume 4:32-5:1-11 & 2 Mambo ya Nyakati 20-22 2-year bible reading plan Luka 1:39-56 & Kumbukumbu la Torati 12 WhatsApp Chanel for rhapsody Translation : https://whatsapp.com/channel/0029Va9SJ9OHFxP0Xh4KCN3F
🙏 1

Comments