Vice President Tanzania

Vice President Tanzania

112.9K subscribers

Verified Channel
Vice President Tanzania
Vice President Tanzania
June 10, 2025 at 03:44 PM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 10 Juni 2025. Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Umoja wa Mataifa.

Comments