Prime Minister Tanzania

Prime Minister Tanzania

259.0K subscribers

Verified Channel
Prime Minister Tanzania
Prime Minister Tanzania
June 18, 2025 at 04:41 AM
*WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAJUMBE WA MISHENI MAALUM YA KUTATHMINI MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU* _▪️Wazungumzia kuhusu maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025_ _▪️Timu hiyo yaridhishwa na mabadiliko na maboresho ya mifumo na Sera kuelekea uchaguzi mkuu_ _▪️Yafurahishwa na na namna Serikali ilivyojipanga kuhakikisha idadi kubwa ya ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa na uchaguzi_ _▪️Mheshimiwa Waziri Mkuu awahakikishia uchaguzi kuwa wa huru na haki_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa jana Juni 17, 2025 amekutana na Misheni Maalum ya Umoja wa Afrika ya Kutathmini Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025 (Pre-election assessment mission - PAM), Misheni hiyo iliongozwa na Dkt. Phumzile Mlambo-Ngcuka; Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Afrika Kusini akiambatana na Wajumbe wengine takribani 16. Lengo la Misheni hiyo ni kutathmini maandalizi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa ilikuhakikisha misingi ya demokrasia inafuatwa kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia Chaguzi na Utawala (African Charter on Democracy, Elections and Governance. Katika mazungumzo na wajumbe wa Misheni hiyo, yaliyofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu,Magogoni Jijini Dar es Salaam, Dkt. Phumzile amebainisha kuwa Misheni hiyo imeridhishwa na maandalizi yanayoendelea kufanyika kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025. “Tumefurahishwa pia kuona kuna idadi kubwa ya wadau wa siasa nchini na kuridhishwa na mageuzi makubwa hususan ya mifumo na Sera yaliyofanywa na Serikali katika kipindi cha hivi karibuni kuhakikisha kiwango kikubwa cha Wananchi wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi” Aidha, Dkt. Phumzile amebainisha kuwa Misheni imefurahishwa kuona kuna idadi kubwa ya ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa nchini. “Hii ni ishara nzuri kuelekea kuwa na uwiano wa 50/50 katika Uongozi na masuala ya siasa” Pamoja na hayo, imebainishwa kuwa kama ilivyo kwa miaka iliyopita, wanategemea Tanzania itaendelea na utamaduni wake wa kufanya uchaguzi kwa amani “Tumezoea Tanzania kuwa na uchaguzi wa amani hivyo tunaamini itakuwa hivyo pia wakati huu” amesema Dkt. Phumzile. Kwa upande wake, Mheshimiwa Majaliwa ameihakikishia Misheni hiyo kuwa Tanzania imejipanga kufanya uchaguzi huru, haki na amani kama ilivyo miaka yote.
❤️ 👍 😭 🙏 7

Comments