TAFAKARI BIBLIA
TAFAKARI BIBLIA
May 31, 2025 at 10:01 AM
Hatuwezi kuwa wakamilifu—maana sisi ni wanadamu, na wanadamu hujikwaa. Tunaanguka. Tunatenda dhambi. Kutokamilika ni katika asili yetu. Lakini adui ananong'ona gizani, "Umeanguka, kaa chini. Umefanya dhambi, endelea kutenda dhambi." Huo ni uwongo wa kuzimu. Kwakua wito wa Mkristo- Mnazareti-sio kubaki katika uchafu, bali kuinuka, tena na tena, na kukimbia kurudi kwa Baba. Kwa maana mwishowe, Mungu hatakuangalia na kukuuliza, “Kwa nini ulifanya dhambi?” Atauliza, “Kwa nini hukurudi Kwangu?” Hiyo ndiyo tofauti kati ya waliopotea na waliokombolewa. Sio kuanguka-bali kurudi.
Image from TAFAKARI BIBLIA : Hatuwezi kuwa wakamilifu—maana sisi ni wanadamu, na wanadamu hujikwaa....

Comments