
GLOBIFY
June 13, 2025 at 12:02 PM
*Ziara ya Globify Charity Katika Kituo cha Yatima cha Islamic Yatima Foundation, Ilemela Mwanza.*
Globify Charity hivi karibuni ilifanya ziara ya kugusa nyoyo za wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Yatima cha *Islamic Yatima Foundation kilichopo Ilemela, Mwanza.* Katika ziara hiyo, walitoa msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto yatima, yakiwemo vyakula, malazi, vifaa vya shule na nguo. Msaada huu ulikuwa wa thamani kubwa, ukiwa na lengo la kuboresha maisha ya watoto hao na kuwawezesha kufikia ndoto zao kwa ujasiri na matumaini.
*Globify Charity* inatoa wito kwa wadau wote kujiunga na jitihada hizi za upendo ili kusaidia kurejesha tabasamu kwa wenye uhitaji. Kila mchango, wa hali na mali, unaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watoto hawa wanaohitaji msaada.
CEO wa Globify Ndugu Issa Halili anasisitiza wadau kwamba *"Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ni chachu ya maendeleo ya kijamii hivyo huu ni wakati wetu kuungana na kutoa, kwa sababu kupitia hisani, tuna uwezo wa kubadili maisha na kuleta nuru kwenye giza."*
Jiunge nasi kupitia - https://chat.whatsapp.com/BiYVpSHVGt34tTA2eMQA3z
*Globify Charity - Let Love Connect Us.*
*GLOBIFY*