
GLOBIFY
June 17, 2025 at 08:56 PM
*JANIYA WILTIKINSON* ni mama wa mtoto mmoja aitwae ARIA mwenye maradhi ya kifafa yanayomsumbua kwa muda mrefu..wanaishi katika nyumba chakavu sababu ya hali ngumu ya kimaisha...
Haitoshi mwenye nyumba anatishia kumfukuza ikiwa atashindwa kulipa kodi kwa wakati..anamuahudi kwamba siku hiyo atapokea mshahara eneo analofanyia kazi
Basi baada ya kumpeleka mwanae shule ambako huko pia mwanae anapitia manyanyaso kutoka kwa walimu wake JANIYA anamuacha na kuelekea kazini huju walimu wakimshangaa na kumsikitikia ..baada ya muda mfupi akiwa kazini anapokea simu inayomjulisha kuwa ARIA ameumia vibaya baada ya kupata kifafa.
Anaomba ruhusa kwa Bosi wake kwa ukali anamwamuru arejee kazini baada ya dakika 30...anaomba japo apewe mshahara wake akamsaidie mwanae bosi wake anagoma.
JANIYA anakimbilia benki ili kutoa kijipesa kwa ajili ya ARIA lakini account yake ina kiasi kidogo tu ambacho ni kilinda account ambacho anaambiwa hakiwezi kutokewa...sa itakuwaje anaelekea hivyo hivyo shuleni mikono mtupu...baada ya kufika shule anakuta Maafisa wa Huduma za Ustawi wa Watoto wakimchukua ARIA.
JANIYAH anaomba Wasimchukue binti yake lakini hawamsikilizi kwa sababu kashindwa kumuhudumia
Inabidi arudi kazini kwa sababu ndio siku ya malipo na ndio siku aliyoahidi kulipa Kodi...lakini ilikuwa siku ya kufa nyani huko nako anakuta barua ya kufukuzwa kazi.. haitoshi Bosi wake anakataa kumpa mshahara wake...karudi nyumbani, anakuta vitu vyake vimetupwa nje... A hard day to JANIYAH
Anarudi kazini kumbana bosi wake wakiwa wanalumbana, majambazi wawili wenye silaha wanaingia...Mmoja anambana bosi antoe hela Mwingine anataka begi la JANIYAH, lakini JANIYAH anakataa.. Katika mapambano wakigombea begi JANIYAH anajikuta kampiga jambazi risasi.
Bosi wake anamtuhumu JANIYAH kwamba kapanga uvamizi huo... lakini JANIYAH anamwambia Hapana..wakati huo bosi wake anapiga simu polisi..bila kutegemea JANIYAH anamfyatulia risasi na bosi wake kisha anakimbia na check yake ya mshahara na kuacha minoti waliyotaka kuiba wale majambazi na kuelekea benk
Sasa Akiwa bank mkosi Bado unamuandama wahudumu wanagoma kumuhudumia kisa eti hana kitambulisho. Akiwa hana njia nyingine, JANIYAH akatoa bunduki ya wale wahuni... Wahudumu Kuona hivyo wakajua kateka bank upesi wakammwagia mafurushi ya hela..ila yeye akachukua kidogo tu kiasi kilichokuwa kwenye check
Wakati yote hayo yanaendelea alam imepigwa na bank imezungukwa na maaskari na wapelelezi kumkabili gaidi huyo... Kisha wakampigia JANIYAH wakimtaka aachie benk na kujisalimisha...Wakati yote hayo yanaendelea ndani ya bank Kuna mfanyakazi katega simu yake na karusha tukio hilo moja kwa moja mtandaoni
Namna anavyoelezea mapito aliyopitia mpaka kufika hapo...watu wanaotazama tukio hilo live wanaanza kumhurumia na kujikusanya nje ya benki kushinikiza aachwe huru.
Akiwa hapo benki JANIYAH anapokea simu kutoka kwa mama yake, akimwambia kwamba mbona mwanae ARIA alishakufa kitambo kwa kifafa...
Kumbe kwa kipindi chote Cha heka heka na majanga aliyokutana nayo kwaajili ya mwanae ni kwamba ARIA alisha kufa lakini mama yake Kuna shida anayo na kajenga taswira kwamba bado Mwanae yupo hai...hata anapompeleka mwanae shule walimu wanamchora tu wanajua si mzima..
*Fuatilia Tips za movie mbalimbali kupitia* - https://chat.whatsapp.com/FmnyIq7TVi6Hkmd4IN1UNV
*GLOBIFY FILMS*
