LIBRARY OF BOOKS📚📚
LIBRARY OF BOOKS📚📚
May 22, 2025 at 06:25 PM
LIBRARY OF BOOKS 📚 "Mafanikio yako yataanzia pale uwoga wako utakapoishia." Katika kitabu The Mountain Is You cha Brianna Wiest, mlima unaozungumziwa si ule wa miamba na barafu, bali ni mlima wa ndani yako – ule wa hofu, mashaka, maumivu ya zamani, na vizuizi vya kiakili unavyoweka mwenyewe. Ni mlima unaokuzuia kufika kileleni pa ndoto zako. Picha hii inavyoonesha mtu anayepanda juu ya mwamba mkubwa ni mfano halisi wa safari ya ndani ya kila mmoja wetu. Huo mwamba ni uwoga wako – wa kushindwa, wa kutoonekana, wa kutokubalika, au hata wa mafanikio yenyewe. Pale ambapo uamuzi wa kuupanda mlima huo unachukua nafasi ya hofu, ndipo mafanikio yako huanza. Unaposema "sitaki tena kuogopa" na kuchukua hatua – hata ndogo – tayari umeanza kupanda. Na kadri unavyopanda, mwanga unazidi kuonekana. Jiulize leo: "Ni mlima gani ndani yangu ninahitaji kuushinda?" Kisha chukua hatua moja – leo. Mafanikio yako tayari yanasubiri upande mwingine wa huo mlima. Keep learning 🤞 💚 Given by Josiah Nashon – 0766 408 259 https://www.instagram.com/p/DJ9zepmsr3I/?igsh=MXJucmlldTNsemFlNA==
❤️ 1

Comments