MACADAMS JOB OPPORTUNITIES
MACADAMS JOB OPPORTUNITIES
June 16, 2025 at 08:32 AM
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Kampuni: GOLDWISH COMPANY LIMITED Mahali: Kibaha, Mkoa wa Pwani Nafasi: Fundi Mchomeleaji Magari (Nafasi 1) Kampuni ya Goldwish inayojishughulisha na huduma za magari ya usafirishaji na Uundaji wa miili ya magari (bodywork), inakaribisha maombi ya kazi kwa nafasi moja (1) ya Fundi Mchomeleaji Magari. Majukumu ya Kazi: Kufanya kazi ya kuchomelea na kutengeneza miili ya magari. Kutambua na kurekebisha sehemu za gari zilizoharibika au kuathiriwa na kutu. Kusoma na kufuata michoro ya kiufundi na vipimo. Kutumia kwa usahihi vifaa vya kuchomelea na kuhakikisha usalama kazini. Kushirikiana na mafundi wengine katika utekelezaji wa kazi. Sifa za Muombaji: Uzoefu wa angalau mwaka 1 na kuendelea katika kazi za uchomeleaji magari. Ujuzi katika aina mbalimbali za uchomeleaji kama MIG, TIG, na ARC welding. Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na katika timu. Cheti cha mafunzo ya welding kutoka VETA au taasisi inayotambulika (kitapewa kipaumbele). Uaminifu, bidii, na umakini mkubwa katika kazi. Mshahara: Tsh 450,000/= kwa mwezi Jinsi ya Kutuma Maombi: Tuma maombi, wasifu binafsi (CV), na nakala ya vyeti kupitia: Barua pepe: WHATSAPP NO:0714615360 Mwisho wa kutuma maombi:Jumanne, Tarehe 17 Juni 2025, saa 11:59 jioni
🙏 2

Comments