TAKUKURU

TAKUKURU

59.5K subscribers

Verified Channel
TAKUKURU
TAKUKURU
June 18, 2025 at 05:10 AM
*KIKAO CHA 49 CHA AUABC - MHE. KAPERA AAPISHWA:* Kikao cha Kawaida cha 49 cha Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri Dhidi ya Rushwa (AUABC) kinafanyika Jijini Arusha yalipo Makao Makuu ya Bodi hiyo kuanzia Juni 16, 2025 hadi Juni 21, 2025. Katika siku ya kwanza ya kikao hicho, wajumbe wapya wa Bodi akiwemo Mhe Benjamin Kapera kutoka TANZANIA, waliapishwa. Wengine walioapishwa ni Mhe. Dkt Graciano Dominongos (Angola) na Mhe. Absatou Ly Diallo kutoka Senegal. Mhe. Benjamin Kapera kutoka Tanzania ambaye pia ni mtumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU, alichaguliwa kuwa mjumbe Februari 13, 2025 katika mkutano uliofanyika Addis Ababa Ethiopia. Kikao cha 49 kimeenda sambamba na uchaguzi wa na uongozi mpya wa Bodi ambapo Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Mhe. Kwami Senanu kutoka Ghana, Makamu Mwenyekiti ni Mhe. Yvonne Chibiya kutoka Zambia na Katibu ni Mhe. Principe Ntibasume kutoka Burundi. Muda wa uongozi wa Bodi ni miaka 2 ambapo wajumbe wapya wanatarajiwa kutumikia kwa miaka 6.
Image from TAKUKURU: *KIKAO CHA 49 CHA AUABC - MHE. KAPERA AAPISHWA:*   Kikao cha Kawaida c...

Comments