
TAKUKURU
June 19, 2025 at 06:05 AM
*KIKAO CHA 16 CHA WATAALAMU WA UTEKELEZAJI WA UNCAC - VIENNA:*
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki katika kikao cha 16 cha Wataalamu wa Utekelezaji wa 'United Nations Convention Against Corruption - UNCAC', kinachofanyika kwa siku 5, Jijini Vienna - Austria.
Katika kikao hiki Mkurugenzi wa Uchunguzi TAKUKURU Bw. Simon Maembe (katikati), amewasilisha Taarifa ya ujumla ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa mkataba huo lakini pia amewasilisha taarifa ya namna Tanzania tunavyotekeleza suala la ulinzi wa watoa taarifa na mashahidi.
Kutoka TAKUKURU mkutano huu unahudhuriwa na DOI Bw. Simon Maembe pamoja na Gabriella Gabriel kutoka Kurugenzi ya Elimu kwa Umma.
Wengine kutoka Tanzania ni ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Austria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka - Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa pamoja na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.
Mkutano unafanyika Juni 16 - 20, 2025.

👍
1