WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

WIZARA YA FEDHA - TANZANIA

180.2K subscribers

Verified Channel
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
WIZARA YA FEDHA - TANZANIA
June 18, 2025 at 01:38 PM
*DKT. MWAKIBINGA AWATAKA WANAHABARI KUSAMBAZA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MNYORORO WA UGAVI* Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, amewataka wamiliki na wahariri wa mitandao ya kijamii nchini kutumia vyombo vyao kueneza elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa kuwa na usimamizi madhubuti wa mnyororo wa Ugavi nchini. Dkt. Mwakibinga alisema hayo, wakati akifungua mafunzo kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ukumbi wa Mikutano wa 88 Mkoani Morogoro. Dkt. Mwakibinga alisema kuwa kupitia vyombo vya Habari, Serikali itaweza kuwafikia Watanzania wengi, kuweza kuufamu vizuri umuhimu wa usimamizi wa mnyororo wa Ugavi na kujipanga kuusimamia vizuri ili uwe na matokeo yanayotarajiwa kwa wananchi. "Tumeandaa mafunzo haya muhimu ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi (Supply chain management) na kupitia kwenu tungependa kuwafikia wananchi wa Tanzania, waweze kuufamu vizuri huu mnyororo na hivyo kuweza kujipanga kuusimamia vizuri ili ulete matokeo yanayotarajiwa’’ alisema Dkt. Mwakibinga. Dkt. Mwakibinga alisema kuwa mafunzo hayo kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini yamelenga kuwajengea uelewa wa kina na uwezo mahsusi wa kufikisha taarifa sahihi, kwa wakati na zenye kuleta uelewa mpana kwa wananchi. Aidha, Dkt. Mwakibinga aliongeza kuwa shughuli za mnyororo wa ugavi zinaanzia katika upangaji wa mahitaji, ununuzi, ugomboaji na uondoshaji, upokeaji, uhifadhi, usambazaji, hadi matumizi na uondoshaji wa bidhaa, vifaa au huduma, na endapo kutakosekana kwa usimamizi madhubuti katika hatua yoyote kati ya hizi kunaweza kusababisha hasara kubwa kwa Serikali, upotevu wa rasilimali, au huduma duni kwa wananchi. Pia, Dkt. Mwakibinga aliwataka wamiliki wa mitandao ya kijamii na wananchi kwa jumla kutambua athari zinazotokana na kutokuwepo kwa usimamizi wa shughuli zote zilizopo katika mnyororo wa ugavi, kwani kwa kufanya hivyo kutaiweka serikali katika mazingira mazuri ya kutengeneza miongozo na mikakati mbalimbali ya utekelezaji ili kuimarisha usimamizi na hata kuepukana na athari hizo. "Ni muhimu kutambua athari zinazotokana na kutokuwepo kwa usimamizi thabiti wa shughuli zote zilizoko katika mnyororo wa ugavi, ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa, Kwani, kwa kuzitambua athari hizo kunatuweka katika mazingira mazuri ya kutengeneza miongozo na mikakati mbalimbali ya utekelezaji ili kuimarisha usimamizi na hata kuepukana na athari hizo’’. Aliongeza Dkt. Mwakibinga. Dkt. alisema kuwa Wizara ya Fedha kwa kutambua changamoto zilizopo katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi imeona ni vyema kuandaa mafunzo maalum kwa makundi mbalimbali nchini, ambapo imeanza kutoa mafunzo hayo kwa Wahariri wa vyombo vya Habari, pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini. Mafunzo kuhusu usimamizi wa mnyororo wa ugavi yameendeshwa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe.
🙏 👍 😢 5

Comments