
Jance Media📡 🔵
June 14, 2025 at 10:01 AM
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepiga hatua ya kupunguza magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi kutoka asilimia 4.7 mwaka 2016/17 hadi asilimia 4.4 mwaka 2022/23 ikiwa ni mwelekeo sahihi wa kutokomeza maambukizi hayo ifikapo mwaka 2030.
Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema hayo kwenye mkutano wa tano (5) wa mwaka wa 'Abbott Rapid Diagnostics' unaofanyika jijini Dar es Salaam ambao unalengo la kujadiliana juu ya magonjwa ya kuambukiza ambapo wajumbe wametoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini.
Amesema, Tanzania imepiga hatua katika utekelezaji wa malengo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) ya 95-95-95, uwiano wa watu wanaofahamu hali yao ya VVU miongoni mwa wanaokadiriwa kuwa na VVU umeongezeka kutoka asilimia 65 mwaka 2016/17 hadi asilimia 83 mwaka 2022/23.
"Uwiano wa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU umeongezeka kutoka asilimia 94 mwaka 2016/17 hadi asilimia 98 mwaka 2022/23, na waliopata kufubaza virusi (viral suppression) wameongezeka kutoka asilimia 87 hadi asilimia 94 katika kipindi hicho," amesema Waziri Mhagama
#dondoozaafya

👍
🙏
3