Jance  Media📡  🔵
Jance Media📡 🔵
June 14, 2025 at 10:03 AM
*🌸 ‼️LISHE BORA KWA MAMA MJAMZITO – TRIMESTER KWA TRIMESTER‼️ 🌸* Je, wajua kuwa kila hatua ya ujauzito ina mahitaji yake ya lishe? Usile tu ovyo – kula kwa ajili ya uhai wa mtoto! ✳️ TRIMESTER NI NINI? Ujauzito hugawanyika katika vipindi vitatu (3) vinavyoitwa trimesters: Trimester ya Kwanza (Wiki 1 - 12) Trimester ya Pili (Wiki 13 - 26) Trimester ya Tatu (Wiki 27 - 40) Kila hatua ina mahitaji maalum ya virutubisho kwa ajili ya ukuaji salama wa mtoto tumboni 🤰💕 *🔹 TRIMESTER YA KWANZA (Wiki 1–12)* 👉 Mtoto anaanza kutengenezwa: moyo, ubongo, uti wa mgongo ✅ LISHE MUHIMU: ✔️ Folic Acid – kusaidia ukuaji wa ubongo ✔️ Iron – kuzuia upungufu wa damu ✔️ Matunda yenye Vitamin C – kusaidia kufyonzwa kwa madini ❌ Epuka vyakula vyenye harufu kali kama vinaongeza kichefuchefu *🔹 TRIMESTER YA PILI (Wiki 13–26)* 👉 Mtoto anaanza kuzunguka, mifupa inatengenezwa ✅ LISHE MUHIMU: ✔️ Calcium – kujenga mifupa na meno ya mtoto ✔️ Protein – kwa ukuaji wa misuli na viungo ✔️ Omega 3 – kusaidia akili ya mtoto (kupatikana kwenye samaki, karanga) ❌ Epuka vinywaji vyenye caffeine kama kahawa/soda nyingi *🔹 TRIMESTER YA TATU (Wiki 27–40)* 👉 Mtoto ananenepa, mapafu na kinga vinaimarika ✅ LISHE MUHIMU: ✔️ Wanga wa kutosha – kumpa mama nguvu ✔️ Fiber – kusaidia usagaji chakula (kuepuka kuvimbiwa) ✔️ Iron & Vitamin D – kuhakikisha mtoto hapati upungufu wa damu wala rickets ❌ Epuka vyakula vya mafuta mengi – huchangia kuongeza uzito kupita kiasi *🔔 USHAURI WA KITAALAMU:* 🔹 Kunywa maji ya kutosha (glasi 8–10 kwa siku) 🔹 Kula mara 5 kwa siku kwa sehemu ndogo ndogo 🔹 Hakikisha unatakiwa na daktari/mtaalamu kuhusu virutubisho vya ziada 🌟 Mama, lishe yako ni msingi wa afya ya mtoto wako! Ukipata ushauri wa lishe, mimba itakuwa salama na mtoto atazaliwa mwenye afya njema! 📞 Kwa ushauri wa kitaalamu na virutubisho salama vya mjamzito: Wasiliana nami kupitia WhatsApp: 0612766711 🌱Pata tiba – Afya salama kwa mama na mtoto! 🌱
Image from Jance  Media📡  🔵: *🌸 ‼️LISHE BORA KWA MAMA MJAMZITO – TRIMESTER KWA TRIMESTER‼️ 🌸* Je,...
👍 😢 🙏 3

Comments