
Jance Media📡 🔵
June 18, 2025 at 08:53 AM
Baada ya mapumziko mafupi basi leo Juni 18, Ligi Kuu ya NBC inarejea kwa kupigwa michezo ya mzunguko wa 29 huku mechi zote 8 zikichezwa kwa wakati mmoja katika viwanja mbalimbali na zikitarajiwa kuanza saa 10 jioni.
Michezo itakayotazamwa sana ni ile miwili ya timu za juu zinazogombea ubingwa, Simba wakiwa ugenini pale Ali Hassan Mwinyi, Tabora kukipiga na KenGold ambao tayari wameshuka daraja wakati huo huo Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Young Africans.
Huku zile za chini ya msimamo zikijikwamua kushuka daraja na kucheza PlayOffs:
KMC 🆚Mashujaa FC
Coastal Union🆚Fountain Gate
Namungo🆚Kagera Sugar
Pamba Jiji🆚JKT Tanzania

👍
2