Samawati Safari
Samawati Safari
June 17, 2025 at 07:51 PM
Romulus na Remus walikuwa watoto wa Rhea Silvia binti wa mfalme wa Alba Longa na mungu wa vita, Mars. Baada ya kuzaliwa, walitupwa kwenye Mto Tiber kwa amri ya mfalme Amulius, ambaye alihofia kuwa wangekuwa tishio kwa utawala wake. Hata hivyo, walinusurika na kuokotwa na loba aliyewanyonyesha na kuwalea katika pango la Lupercal lililoko kwenye kilima cha Palatine. Baadaye waligunduliwa na mchungaji Faustulus ambaye aliwalea pamoja na mke wake Acca Larentia. Romulus alikuja kuwa mwanzilishi wa mji wa Roma mnamo mwaka 753 kabla ya Kristo
Image from Samawati Safari: Romulus na Remus walikuwa watoto wa Rhea Silvia binti wa mfalme wa Alb...
👍 1

Comments