Samawati Safari
Samawati Safari
June 18, 2025 at 06:15 AM
Aliongoza shughuli za ndani kwa ustadi mkubwa wakati Mwalimu Nyerere akihusika zaidi na masuala ya kivita na kimataifa. Alihakikisha kuwa raia wanapata huduma muhimu, aliwahimiza Watanzania kujitolea kwa taifa lao, na alijenga taswira ya kiongozi mchapakazi asiyejificha nyuma ya heshima ya cheo Baada ya vita, nchi iliingia kwenye kipindi kigumu cha kiuchumi, ambapo matumizi makubwa ya kijeshi yalikuwa yamepunguza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi. Katika kipindi hiki, Sokoine alijitahidi kusimamia mipango ya kuokoa uchumi huku akikumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya watendaji serikalini waliokuwa wakijihusisha na ufisadi. Alikuwa hana muhali katika kushughulikia maovu, jambo lililomletea heshima kubwa kwa wananchi lakini pia kumletea maadui wengi wa kimfumo. Katikati ya misukosuko hiyo, alijiuzulu mwaka 1980 kwa sababu binafsi. Wengi walihuzunika na hatua hiyo, lakini haikupita muda mrefu kabla ya kurejeshwa tena katika nafasi ya Waziri Mkuu mwaka 1983.
Image from Samawati Safari: Aliongoza shughuli za ndani kwa ustadi mkubwa wakati Mwalimu Nyerere a...
🔥 2

Comments