
Samawati Safari
June 18, 2025 at 06:15 AM
Aliporudi, alionekana kuwa na msukumo mpya wa kupambana na maovu ya kiutendaji yaliyokuwa yameota mizizi.
Alianzisha kampeni kali ya kupambana na rushwa, uzembe, ubadhirifu wa mali ya umma na uonevu kwa wananchi.
Katika kipindi chake cha pili, alizidi kujitokeza kama kiongozi wa mabadiliko na alichukuliwa kuwa kiongozi wa matumaini mapya kwa Tanzania.
Changamoto kubwa aliyokuwa akikumbana nayo ilikuwa ni mifumo ya kiutawala iliyokuwa imesheheni urasimu na baadhi ya watu waliokuwa hawataki kuona mabadiliko.
Hakuogopa kupambana na vigogo waliokuwa wakikwamisha maendeleo.
Alijijengea taswira ya mtu asiye na hofu, anayesema ukweli kwa uwazi, na anayechukua hatua haraka kwa maslahi ya taifa.
Katika harakati zake hizi, aligusa masilahi ya watu wengi waliokuwa wamenufaika na mfumo wa kifisadi.
Alikuwa kama mwiba kwao.
Lakini ghafla, kabla hajakamilisha safari yake ya mageuzi, taifa lilipatwa na mshtuko mkubwa.
Tarehe 12 Aprili 1984, taarifa zilifika kwamba Waziri Mkuu Edward Sokoine amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro, akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.
Habari hizo zilienea kwa kasi kama moto wa nyikani, zikiambatana na mshangao, huzuni na maswali mengi yasiyo na majibu ya moja kwa moja.
Ajali hiyo ilihusisha msafara wa magari, lakini gari la Sokoine pekee ndilo lililopata ajali mbaya.
Wananchi wengi walishindwa kuamini kuwa ilikuwa ajali ya kawaida, na nadharia mbalimbali zilitolewa kuhusiana na chanzo halisi cha kifo chake.
🔥
2