
Samawati Safari
June 18, 2025 at 08:46 PM
🥤La Recta Provincia utawala wa giza usionekana
Jamii hii haikuwa ya kawaida. Ilikuwa na rais, jeshi, baraza la siri, sheria zao, na hata gereza lao – lakini yote yalifanyika gizani.
🥤Serikali hii ya siri ilikuwa na kila kitu:
---Rais (Mkuu wa Wachawi)
......Mawaziri (Watendaji wa Uchawi)
......Mahakama ya wachawi (kuhukumu waliokiuka sheria za kichawi)
......Jeshi lao — viumbe wa kichawi waliokuwa tayari kutumwa…
🥤Wachawi hawa walidai kuwa wanaendesha serikali halali inayotawala Chiloé kisiri.
Wanaaminiwa walikuwa na uwezo wa:
.... Kupaa hewani kwa kutumia mifupa ya wafu.
.... Kuzungumza na mizimu.
... Kubadilika kuwa wanyama kama vile mbwa mweusi au paka mwenye macho mekundu.
.... uweza kuua kwa fikra tu bila kugusa mtu.
.
.... Kutembea bila kuonekana hata kama n mchana
🥤El Imbunche – Mlinzi Mchawi
Kati ya hadithi za kutisha zaidi za La Recta Provincia ni kuhusu mnyama aitwaye Imbunche.
Imbunche hakuwa mnyama wa kawaida.
🥤Alikuwa mtoto mdogo aliyetekwa, akavunjwa viungo vyake vyote, ulimi ukatolewa, na kichwa chake kufungwa upande mmoja ili asitamke siri zozote.
Baadaye alifanywa kuwa mlinzi wa pango la wachawi, akitambaa kwa mguu mmoja na kutisha kila aliyejaribu kuingia bila ruhusa.
Imbunche alikuwa anammaliza kikatili sana.
❤️
1