
Samawati Safari
June 19, 2025 at 09:20 AM
Mapinduzi ya kwanza ya kijeshi nchini Burkina Faso yalitokea tarehe 24 Januari 2022, ambapo jeshi lilimuondoa madarakani Rais Roch Marc Christian Kaboré.
Mapinduzi haya yaliongozwa na Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, ambaye alitangaza kuundwa kwa kundi la kijeshi linaloitwa “Mouvement Patriotique pour la Sauvegarde et la Restauration” (MPSR).
Jeshi lilitangaza kusitishwa kwa katiba, kuvunjwa kwa serikali na bunge, na kuweka marufuku ya kutotoka nje usiku.
Mapinduzi haya yalichochewa na hali mbaya ya usalama nchini, hasa kutokana na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu kama vile al-Qaeda na Islamic State, ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwafanya mamilioni kuwa wakimbizi wa ndani.
Wanajeshi walilalamikia ukosefu wa vifaa vya kijeshi na msaada wa kutosha kutoka kwa serikali katika kupambana na waasi.
Tukio la kuuawa kwa askari 53 katika shambulio la Inata mnamo Novemba 2021 lilikuwa kichocheo kikuu cha mapinduzi haya.
Kipind hicho nchi haeleweki wapigaji ni wengi, nchi inaenda la manyani tu.